ProZ.com translation contests »
32nd Translation Contest: "Movie night" » English to Swahili » Entry by Shalyn Ndombi


Source text in English

Translation by Shalyn Ndombi (#37447) — Winner

To say that I was compelled by Parasite from start to finish is an understatement; its filming style with tracking shots are enthralling. Having watched several Korean films during the London Korean Film Festival, I was familiar with the usual genres employed in such films but Parasite seemed to defy them all! Parasite is comedic, in a quirky way, it is also a thriller, straddles class divisions and also depicts a family tale amongst other genres and is therefore likely to appeal to all ages.

Parasite truly deserves to be watched in a cinema to appreciate its nuances and the stylish cinematography. As a summary, to avoid spoilers, Parasite tells the tale of the interaction between the Park family and the Kim’s, an unemployed family, whose contrasting worlds collide with long lasting consequences.

[...]Bong Joon-Ho manages to pique the audience’s interest with brightly lit shots coupled with the effective use of indoor space, and it is surprising to realise, after the film’s 2 hour 12 minute length, that most of the scenes occur within the Park family’s home. The mundane elements of domesticity are displayed with an intriguing perspective showcasing Bong Joon-Ho’s flair. It is a slow burner but you will revel in its beauty and ingenuity as Parasite convinces that it operates solely on one level but it is in fact multi-layered and depicts social realism with empathy and pathos.

The cast are beguiling to watch, every facial movement and action is accentuated, even the mere act of walking up or down stairs can convey hidden meaning, which the camera fragments. Levels of unease are also created by virtue of that effective use of space with unusual camera angles and dramatic weather conditions ratcheting up that sensation. There is a surreal nature to Parasite, which its score emphasises, and furthermore the film adopts elements of the absurd devised in such an ingenious way which is truly cinematic magic. Parasite’s apparent eeriness will certainly keep you riveted and would not feel alien to the Twilight Zone school of filmmaking.

The actors are very impressive and add breadth to their roles creating relatability whilst seeming effortlessly cool. When Ki-Woo and Ki-Jeong Kim were working within the Park family home as private tutors they certainly epitomised this level of nonchalant, understated authority creating an aura of mysticism with the unspoken, almost mythical, tutoring techniques employed. Quite simply, the actors Park So-Dam and Choi Woo-Sik, as Ki-Woo and Ki-Jeong, are compelling to watch in the different directions that Parasite follows and they carry these performances seamlessly thereby inviting the audience to be on their side.

[...]Parasite is a remarkable piece of extremely skilful filmmaking, it is simply a must see film, and so I am looking forward to re-watching the film on its UK general release date.
Kusema nilivutiwa na filamu ya Parasite kutoka mwanzo hadi mwisho ni hakutoshi kuelezea hali halisi niliyoishuhudia kwa kuitazama filamu hiyo; mtindo wake wa kurekodi filamu na picha za kufuatilia unasisimua. Kutokana na uzoefu wangu wa kutazama filamu kadhaa za Korea wakati wa Tamasha la Filamu la Korea huko London, nilikuwa na ufahamu wa tanzu za kawaida za muziki zinazotumiwa katika filamu hizo lakini filamu ya Parasite ilionekana kuzipiku zote! Filamu ya Parasite ni ya kuchekesha,kwa njia ya kipekee, pia ni kusisimua, inavuka mipaka ya daraja za jamii, na pia inachora hadithi ya familia miongoni mwa aina nyingine za tanzu, na kwa hiyo inaweza kukubalika kwa watu wa umri wote.

Kwa hakika filamu ya Parasite inastahili kuangaliwa kwenye sinema ili kuthamini ubora wake wa kipekee na uigizaji wa kisanii. Kimuhtasari, ili kuepuka kufichua siri za filamu, filamu ya Parasite inaelezea hadithi ya mwingiliano kati ya familia ya Park na familia ya Kim, familia isiyokuwa na ajira, ambazo dunia zao zinazotofautiana zinakutana na matokeo ya kudumu.

[...]Bong Joon-Ho anafanikiwa kuchochea hamu ya watazamaji kwa picha zenye mwangaza mzuri zinazooana na matumizi mazuri ya nafasi iliyomo ndani ya nyumba, baada ya filamu yenye urefu wa masaa 2 na dakika 12 inashangaza kugundua kwamba sehemu kubwa ya matukio yanatokea ndani ya nyumba ya familia ya Park. Vipengele vya kawaida vya maisha ya nyumbani vinaonyeshwa kwa mtazamo wa kuvutia ukionyesha ustadi wa Bong Joon-Ho.Ina mwendo wa taratibu lakini utafurahia uzuri wake na ubunifu wa filamu ya Parasite ikishawishi kuwa inafanya kazi kwa ngazi moja pekee lakini kwa kweli ina matabaka mengi na inachora uhalisia wa kijamii kwa hisia na huzuni.

Waigizaji wanavutia kuitazama, kila mwendo wa uso na hatua inaonekana, hata tendo la kawaida la kupanda au kushuka ngazi linaweza kutoa maana iliyofichika, ambayo kamera inapakia. Viwango vya taharuki pia vinajengwa kutokana na matumizi mazuri ya nafasi ndani ya chumba na pembe za kamera zisizo za kawaida kwenye maeneo isiyozoeleka pamoja na hali ya hewa yenye drama, ikiongeza hisia hiyo. Filamu ya Parasite ina ina mvuto usio wa kawaida, ambayo inatilia mkazo na zaidi ya hayo, filamu hii inachukua vipengele vilivyoundwa kwa njia yenye ubunifu ambayo ni mazingaombwe ya sinema ya kweli. Maajabu yanayayojitokeza kutoka uigizaji wa filamu ya Parasite utahakikisha unanatwa kuitazama na haitaonekana kama kitu kigeni kwa mtindo wa utengenezaji filamu wa shule ya Twilight Zone.

Waigizaji wanavutia sana na kuongeza upana kwenye majukumu yao, wakiunda uhusiano wa kufanana huku wakionekana kuwa na mtindo wa kupendeza bila jitihada
Wakati Ki-Woo na Ki-Jeong Kim walikuwa wakifanya kazi ndani ya nyumba ya familia ya Park kama walimu wa binafsi, bila shaka walidhihirisha kiwango hiki cha utulivu, mamlaka tulivu kuunda mandhari ya mafumbo na mbinu za kufundishia zisemwazo, karibu za hadithi, mbinu za ufundishaji zilitumika. Kwa ufupi, waigizaji Park So-Dam na Choi Woo-Sik, kama Ki-Woo na Ki-Jeong, wanavutia kuwatazama katika mwelekeo tofauti ambao filamu ya Parasite inafuata na wanaufanya uigizaji kuonekana mwepesi bila ugumu hivyo kuwavutia watazamaji kuwa upande wao.

[...]Filamu ya Parasite ni filamu ya kipekee ya kukumbukwa iliyotengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu wa uundaji wa filamu, ni filamu ambayo lazima uione, na kwa hivyo natarajia kuiona tena siku ya kutolewa rasmi nchini Uingereza.


Discuss this entry